Tusipo vipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, Nani avipongeze?

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on print

April 29th, 2021. Mch. Dkt. Peter Bujari


Nimekuwa nasikia moyoni mwangu ile sauti ya Hayati JPM ikisema “Hii ni vita ya uchumi” na mara kadhaa nimeona watu wanabeza usemi ule. Pamoja na kwamba 

wanazo sababu zao za kubeza, na sitaki kuwazungumzia hao, kuna jambo limenifikilisha sana mpaka nimetamani kuandika leo. Wale wanao nifahamu, wamesikia mara kadhaa nikisema kuwa wazungu wanatupenda kwa lipi mpaka watusaidie kama hakuna masilahi yao?.

April 21, 2021 tulianza kupata taarifa za kimbunga kikitokea mashariki ya kisiwa cha Madgasca na kutegemewa kuathiri Zanzibar na Dar Es Salaam. 

Chombo cha Habari CNN kilitangaza kuwa kimbunga hicho ni kibaya kutokea na kuwa cha mwisho kilikuwa mwaka 1952. Miaka hii mimi sijazaliwa hivyo ina maana sijawahi kukiona wala kikisikia.

Hii taarifa ilileta taharuki miji ya lindi, Mtwara, Zanzibar na Dar Es Salaam. Baadae mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) ikatangaza kuwa kimbunga hicho kiingefikia nchi kavu Jumapili ya tarehe 25 April 2021. Tuliambiwa tusiendeshe magari Jumapili hiyo. Wakati huo huo, ilishauriwa kuwa usafiri wa majini usitishwe ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza. Shirika la Aljazeera lilitangaza lilimrukuru Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa ya Tanzania kuw alionya wavuvi kusitisha shughuri zao mpaka kimbunga kipite.

Siku moja kabla ya siku iliyotangazwa kimbunga kufika ( April 24), Kamishina wa kuzuia madawa ya kulevya Bwana Gerald Kusaya akatoa taarifa za kukamatwa shehena ya madawa ya heroine ikiingia Kilwa mkoani Lindi. Kamishina anasema madawa hayo ni Zaidi ya tani moja na watu saba walikuwa wamekamatwa.

Baada ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kukamata mzigo huo, Jumapili ya tarehe 25.04.2012 tukatangaziwa kuwa kimbunga Job kimekutana na upepo kinzani na kuwa kimeishiwa nguvu. Ikafahamika pia kuwa kimbunga hicho hakitakuwapo tena. Najiuliza je kuna uhusiano kati ya taarifa za Kimbunga Jobo na kuingizwa kwa madawa ya Heroine Tanzania? Je kama ulinzi ungesimamishwa majini madawa haya si yangeingia?. Je huu ni mradi wa nani na yuko wapi?

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughurikia madawa ya kulevya UNOC lilikadiria kuwa kwa mwaka 2016 bei ya heroine mtaani ilikuwa dola 56 kwa gramu moja. Tumeambiwa kuwa madawa yaliyokamatwa ni Zaidi ya tani moja. Tuchukulie ni tani moja, ambayo ni kilo 1,000. Kilo moja ina gramu 1000, hivyo tani moja ni gramu million moja. Kwa hiyo tani moja ya heroine ni sawa na dola za kimarekani million hamsini na sita ( $56,000,000) kwa bei ya rejareja. Hii bishara siyo ya kitoto ni ya wakubwa wasioipenda Tanzania bali hupenda masilahi yao tu. Na wewe takakari kama mimi, bado sijapata majibu. Kama kiongozi katika taifa hili, najiuliza watu wa aina hii wanaitakia Tanzania nini?

Nachukua nafasi hii kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama na kuwaombea kwa Mungu wetu awape hekima Zaidi kufanya kazi kwa weledi Zaidi.

Mungu ibariki Tanzania.

8 thoughts on “Tusipo vipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, Nani avipongeze?”

 1. Kwa kweli Umeandika Ujumbe Mrefu lkn wenye mapana makubwa Wewe ni tunu ya Taifa Kuanzia leo naanza kufuatilia makala zako

 2. Frank Metusera

  Kwa hakika nimeona mwangaza kupitia hili andiko na kupata imani kwa yeye aliyeliandika Tunawasubiri watu wenye kuona maono makubwa na yenye imani kuwa viongozi wa taifa letu Na mm niseme nanza kufuatilia makala zako

 3. Desdery Peter

  Kwa hakika umenifungua akili maana kuna mambo mengine yalitokea ila sikuyatazama kwa jicho la ndani, nimejifunza kumbe kuna mambo mengi yanafanyika ndani ya nchi hii yenye kuiathiri, ila sisi tunayachukulia kawaida tuu, asante sana Dr

 4. Lwitiko R Ndagile

  Kiukweli nchi zetu bado zipo kwe ukoloni ambao ni ukoloni mamboleo, ambao umejikita zaidi katika kutawaliwa kiuchumi na kufanya kuwa na nchi ambazo zina Uhuru wa bendera (flag Independence), ndomana wazungu wanatugandamiza tusiweze kujitegemea, kisha wanatusaidia na kwa mtu asie elewa anawapongeza, Hongera sana kwa makala nzuri MUNGU akubariki.

  1. Peter Bujari MD

   Afrika ni bara lililotengwa na Mungu kwa ajili ya baadae. Tunahitaji viongozi wenye miiko kutufikisha hapo

 5. Hi,

  Struggling to reach more customers and boost your sales in the competitive online market?

  Without a user-friendly and attractive e-commerce website, you might be missing out on significant opportunities to grow your business and enhance your brand visibility.

  At OutsourceBPO, we create stunning, custom e-commerce websites designed to meet your unique business needs. Here’s how we can help:

  – **Custom Design:** Reflects your brand’s identity.
  – **User-Friendly:** Easy navigation on all devices.
  – **Essential Features:** Secure checkout, customer accounts, and more.
  – **SEO & Marketing:** Optimized and integrated to drive sales.
  – **Ongoing Support:** Continuous maintenance and updates.
  – **Affordable Pricing:** Packages to fit your budget.

  Let’s schedule a free consultation to discuss your goals and how we can help you achieve them. Visit https://outsource-bpo.com/website/?peterbujari.com for more details .

  Best regards,
  Sam

 6. Hey

  The New Powerful LED Flashlight is The Perfect Flashlight For Any Situation!

  The 3,000 Lumens & Adjustable Zoom gives you the wide field of view and brightness other flashlights don’t have.

  50% OFF + Free Shipping! Get it Now: https://linterna.cc

  Sincerely,

  Simon

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *