Wanaoongoza wasipofanya wajibu wao wananchi watajifunza wapi?

Dar Es Salaam. Novemba 13, 2022.  Mch. Dkt. Peter Bujari


Ni jioni ya jumapili mchana nikiwa jijini Accra nchini Ghana, tarehe 6 Novemba nikijiandaa kuwasilisha mada kwenye mkutano wa kimataifa unaojadili maswala ya uwekezaji katika Sekta ya afya  hususani huduma za Mama na mtoto. Mada yangu ilikuwa namna Tanzania inavyofanya vizuri katika ufadhiri wa sekta ya afya. Shauku yangu na hamu iliiingia simanzi aliponiuliza mwenzangu kutoka Kenya kama nilikuwa na taarifa za ndege iliyoanguka?

Sambaza kwenye mitandao mingine
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on email
Share on telegram

Dakika chache baadae nilitumiwa picha iliyoonyesha ndege ikiwa majini na ikiwa inavutwa kwa Kamba na wananchi waliojipanga mstari mrefu. Rafiki yangu mmoja alinitonesha pale aliponiuliza kwa kingereza kuwa “ Nchi kama yenu hata winchi hamna kuvuta ndege mnatumia Kamba”. Moyo wangu ulikufa ganzi na nilishindwa cha kujibu, nikamwambia kuwa ningefuatilia, pengine ni mambo ya mitandaoni kutengeneza picha, binafsi sikuamini kama ndege inavutwa kwa Kamba.

Pamoja na kuwa kuna ajali nyingi zimetokea miaka ya nyuma, naomba kurejea ajali mbili ambazo kama nchi zinatuvua nguo na kuonyesha kuwa wanaoongoza ama hawajui ama hawafanyi wajibu wao.  

Mbaya Zaidi binafsi sijaridhika na hatua zinazochukuliwa na wanaoongoza katika mambo haya na ndiyo sababu ya kuandika Makala hii.

May 21, 1996 nilikuwa jijini Mwanza nikijiandaa Kwenda chuo kikuu pale ambapo meli ya MV Bukoba iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 430 ilipoua watu karibu watu 1,000 zaidi ya mara mbili ( Kwa mujibu wa Wikipedia). Taarifa zinasema daraja la kwanza na la pili zilionyesha kuwa meli ilibeba abiria 443 lakini daraja la tatu hawakujulikana abilia waliokuwemo. Mtaalamu mshauri wa mambo ya majini Joseph Muguthi aliyefanya uchunguzi alisema “ilikuwa ni ajali inayosubiriwa kutokea” kwa maana taratibu za kiusalama zote hazikuzingatiwa akishutumu serikali kuwa iliajili watumishi wasio na ujuzi stahiki. Ukosefu wa vifaa vya uokozi na uokoaji, kiasi waokoaji kutoka Afrika ya Kusini walilazimika kufika Tanzania. Swali langu ni kuwa Je wanaoongoza nchi hii walijifunza nini katika janga lile na wakaweka mikakati gani?

Miaka 27 baadae ndege mali ya Precision Air imelazimika kutua ndani ya ziwa Victoria, umbali kati ya mita 100- 500 na kuwa ilizunguka angani kati ya Mjini Bukoba, wilaya za Muleba na Misenyi kwa takriba ni nusu saa. Ajabu ni kuwa ndege ilipoanguka hakukuwa na uokozi wa kitaalamu isipokuwa wananchi wa kawaida na wavuvi kama ilivyokuwa miaka ishirini na saba iliyopita. Je wanaoongoza wanajua wanachokifanya? Je wanajua wajibu wao? Na kama hawajui wajibu wao, wananchi watajifunza wapi?.

Wataalamu wa uongozi kama Philipe Joubet Mwanzilishi na mkurugenzi wa “Earth on board” na wengine husisitiza kuwa viongozi  wanahitaji kuwa na malengo ya muda murefu ili kuruhusu ubunifu na kuongeza ufanisi katika kazi. Bwana Joubet anasema ubunifu siyo mpango wa Mungu, bali huja kwa kuwa na lengo la muda murefu. Je Mipango ya muda murefu ya viongozi wetu katika majanga na uokoaji ni ipi?. Bahati mbaya Tanzania tumeamini katika viongozi wa-kisiasa ambao malengo yao ni kushinda uchaguzi ujao. Kwa uchambuzi wangu, viongozi hawajajifunza kwa miongo mitatu, je tutaendelea hivi mpaka lini?. Nashauri viongozi waliopewa dhamana wajitathimini juu ya uongozi wao na wawajibike. Vinginevyo hakutakuwa na mabadiliko yoyote.

Wasiliana nasi bujari@peterbujari.com

16 thoughts on “<strong>Wanaoongoza wasipofanya wajibu wao wananchi watajifunza wapi?</strong>”

  1. You’ve written terrific content on this topic, which goes to show how knowledgable you are on this subject. I happen to cover about Coupon Codes on my personal blog Webemail24 and would appreciate some feedback. Thank you and keep posting good stuff!

  2. This is quality work regarding the topic! I guess I’ll have to bookmark this page. See my website Seoranko for content about Search Engine Optimization and I hope it gets your seal of approval, too!

  3. أنابيب GRP في العراق تتخصص شركة إيليت بايب في تصنيع أنابيب البلاستيك المدعمة بالزجاج (GRP)، وتوفير حلول من الدرجة الأولى تلبي مجموعة متنوعة من الاحتياجات الصناعية. تشتهر أنابيب GRP لدينا بقوتها ومتانتها ومقاومتها للظروف البيئية القاسية. تم تصميمها لتحمل الضغوط العالية والمواد الكيميائية القوية، مما يجعلها خيارًا ممتازًا لتوزيع المياه، وأنظمة الصرف الصحي، والتطبيقات الصناعية. من خلال الاستفادة من التكنولوجيا المتقدمة والمواد عالية الجودة، أثبتت شركة إيليت بايب نفسها كمزود رائد لأنابيب GRP في العراق. تميزنا بالتفوق والموثوقية يجعلنا واحدة من المصانع الرائدة في البلاد. استكشف عروضنا على elitepipeiraq.com.

  4. So you may be experiencing stress- induced depression even if you don t suffer from a negative or anxious state of mind during the rest of your day [url=https://fastpriligy.top/]priligy amazon canada[/url]

  5. Metformin attracted cancer researchers attention when it was found to be associated with a lower risk of breast cancer risk in observational studies of diabetic patients, Dr [url=https://fastpriligy.top/]priligy dapoxetine 30mg[/url] methylcobalamin benadryl and weight gain The best advice I have received from U

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *