Mapinduzi ya nne ya viwanda na viongozi tunaowataka

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on print

Masomo ya Uongozi wenye tija (High Impact Leadership) huonyesha kuwa dunia ya sasa imekuwa ngumu isiyotabirika, na hivyo huielezea kwa sifa nne ( Volatile (V), Uncertainty (U), Complex ( C) na Ambiguous (A) kwa ufupi VUCA. Hali hii ya dunia inahitaji viongozi wenye maono ya muda mrefu, wenye miiko (Values) na malengo (Purpose) ya watu wao. Hawa ndio viongozi tunaohitaji kutuongoza katika mapinduzi ya viwanda ya nne (4th industrial revolution) Philipe Joubet Mwanzilishi na mkurugenzi wa “Earth on board”  anasema dunia 

inabadilika kwa haraka sana hivyo viongozi wenye tija wanahitajika kuongoza ubunifu katika mapinduzi ya viwanda ya nne. Anasema viongozi wanahitaji kuwa na malengo ya muda murefu ili kuruhusu ubunifu na kuongeza ufanisi katika kazi. Katika mada yake chuo cha Cambridge, Bwana Joubet anasema ubunifu siyo mpango wa Mungu, bali huja kwa kuwa na lengo la muda murefu na kisha kuhakikisha kuwa viongozi wenzako wanajua na kukubaliana na lengo hilo. Profesa Jaideep 

Prabhu wa chuo kikuu cha Cambridge anasema kuwa mafanikio ya leo ndiyo yanaua ubunifu wa kesho katika viongozi wengi.  Mapinduzi ya viwanda ya nne (4th industrial revolution) yanahitaji viongozi watakaoongoza ubunifu utakao wawezesha watu kufanya mambo makubwa kwa gharama kidogo (Frugal innovation). Viongozi wenye maono ya muda mrefu (Long term vision), ambao hawaendi mbele ya watu bali huhamasisha na kuelewesha watu maono yao (shared vision) ili watembee Pamoja. Masomo ya uongozi wenye tija (High Impact Leadership) huonyesha kuwa viongozi wenye tija wanahitaji watu wengine ili kuongoza na kuwa huweka thamani (Value) katika watu wanaowaongoza (Collaborative leadership).

Hapa Tanzania katika awamu ya nne tuliwekeza sana kwenye umeme ghari wa (generata itumiayo mafuta) na gharama za uzalishaji zilikuwa kubwa. Awamu ya tano ilianza kufufua miradi iliyobuniwa miaka ya 1970 ya kuzalisha umeme kwa maji. Miradi hii inajengwa na mingine inapangwa kujengwa ili kuzalisha umeme wa maji kwa gharama kubwa. Umoja wa mataifa mwaka 2016 ulikadiria kuwa ifikapo mwaka 2030, dunia itakuwa na upongufu wa maji kwa 40% ya kiwango cha wakati ule (SDG6). Je viongozi wetu wanapoamua kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji, wanamaono ya muda mrefu?. Shirika la hali ya hewa duniani linakadiria kuwa kuna uwezekana wa joto la dunia kuongezeka kwa 1.5C katika miaka mitano ijayo. IKiwa maji yatapungua na joto litaongezeka, si vema kuwekeza kwenye kitakachoongezeka?.

Sekta ya usafiri na usafirishaji inategemewa kukumbwa na mabadiliko ya kasi miaka ijayo. Magari mengi sasa yanatumia mifumo ya mafuta yatabadilika na kutumia umeme na gesi ya haidrojeni. Vyuo vyetu vya ufundi imevipasa kubadilika na mafundi pia. Magari yanayotumia umeme na hewa ya hydrojeni yatashika kasi duniani miaka michache ijayo, yafanya nishati ya mafuta kupungua bei na kupoteza soko. Tanzania inajenga bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga. Magari ya umeme hutumia madini makubwa matatu ya Cobalt, Lithium na Nickel yote yanapatikana Tanzania. Viongozi wenye tija Tanzania wanahitajika kuongoza maandalizi si tuya kutumia hizi rasilimali, bali kuwaandaa watanzania kunufaika na mapinduzi haya. Kiongozi mwenye tija anakuwa tayari kufuta yale aliyokuwa anayajua na kuweka mengine mapya (Learn and de-learn). Je viongozi hao tunao?

Nipe mawazo yako kupitia successadvisor@peterbujari.com  

34 thoughts on “Mapinduzi ya nne ya viwanda na viongozi tunaowataka”

 1. Sospeter Aloyse

  Kwa mtazamo wangu kwanza nianze kusema kwamba sina hakika kama viongozi ao tunao ila labda naweza kuona kwamba Magufuli alijaribu kufanya kitu chenye tija kwa kufufua miradi hiyo ya miaka ya 70. sijui kama mawazo yangu yako sawa

 2. Geoffrey Msando

  Mimi nina swali nini maana ya maono na mtazamo maana yake ni nini? nitashukuru nikiyafahamu hayo kwa undani.

  1. Peter Bujari MD

   Bwana Godfrey Salaam. Asante kwa swali lake. Maono na mtazamo ni vitu viwili tofauti Kabisa. (1) Mtazamo ni namna mtu anavyoona na kutafsiri mambo. Mara nyingi mtazamo wa mtu hutegemea na miiko (Values) zake. Mtu anaweza kuwa na mtazamo hasi kutegemea na uzoefu wake wa Nyuma. Kwa upande mwingine (2) Maono ni hali ya baadae katika picha ambayo mtu au jamii hutaka kufikia kipindi kijacho. Wengine huita ndoto. Mani, mwanafunzi anaweza kuwa na maono ya kuwa daktari. Maono humzuia mtu kufanya mambo yasiyompeleka kwenye maono yake. Hivyo mwanafunzi atajizuia kufanya mambo yatakayomfanya asiwe daktari. Maono humkosesha mtu usingizi mpaka ayafikie.

   Natumaini umeona tofauti yake. Tuendelee kuelimishana

 3. Ramla Mahamudu

  Jana Mwenge wa uhuru ulipita hapa Tanga kwenye uzinduzi wa kituo cha Sayansi ambacho na mimi nimeshiriki katika ujenzi wake, hapa tunao mradi wa kuzalisha umeme kutoka kwenye betri za laptop na takataka nyingine zenye kemikali lakini nimekuwa naona mwitikio mdogo wa serikali katika kuwezesha miradi kama hii mwisho wasiku tunafanya wenyewe kwa nguvu zetu, Niliposoma Makala hii sasa nimeelewa ni kwa nini serikali yetu inakwama, kwa kumalizia swali langu ni je? Ikiwa tayari tuna viongozi wasio na maono ya muda mrefu katika kipindi hiki tufanye nini ili hatima yetu isiharibike.

  1. Peter Bujari MD

   Bwana Ramia nakuelewa Kabisa. Nilimsikia PM akisema wabunifu wataendelezwa Latino Hakuna Mkakati na hakuna bajeti. Wanaopewa baker Hugo (Tume ya Sayansi na Tekolinologia) hawana mkakati wa muda INCUBATIO kulea wabunifu wa sayansi mpaka kitu wanachofanya kiweze kutumika kwa kiasi kikubwa na kwa ubora. Mfano wa mradi wenu wa renewable energy ni ubunifu mkubwa wa kuungwa mkono, kuendelezwa na kuwa-scalable.

   Bahati mbaya viongozi wengi hawana malengo ya muda Murefu, kusudi na miiko. Kila wakati huuliza nitapata nini. Haya ni mawazo mafupi. Kiongozi mwenye tija hujiuliza NITAACHA ALAMA gani kukumbukwa?

   Turndelee kuelimishana

   1. Ramla Mahamudu

    Asante sana Daktari mm ni mwanamke naitwa Ramla tangu nilipoingia kwenye Website hii nimepata shauku ya kukufuatilia sana na nimewiwa kujifunza kwako, naamini watu kama ninyi ni viongozi wazuri na wenye maono ya muda mrefu yanayoweza kumsaidia na kumgusa kila mmoja. Mwenyezi Mungu akubariki sana

 4. Anord Alphonce

  Mweshimiwa mama Samia Suluhu Hassan naomba akupe cheo cha waziri wa mipango tafadhali nimevutiwa sana hii imekaa kisomi sana.

 5. Juma Atwibu Wa Mtwara, kwanza kabisa ombi langu na mimi ni kuwaomba viongozi waitazame stand yet hapa Nanyamba naomba serikali mtukumbuke Je, swali langu ni kwamba inawezekana kukosa ruti nyingi za kwenda maeneo mengi ni sababu ya kutokuwa na stand yenye mazingira rafiki kwa abiria na wamiliki wa vyombo vya usafiri na kama ni ndiyo je maswala ya ujenzi kama stend n.k nayo yanahitaji maono ya muda mrefu

 6. Nimekutana na hii Article nikiwa nasoma ahabri lakini nilipo ona kichwa cha habari kuhusu viwanda nimekuja kulifuatilia lakini hii Article imenifany nikufuatilie post Nyingine zote na nimegundua mwandishi ni mtu mwenye iq kubwa

 7. Faustine James

  Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza mwandishi wa hii makala lakini pia nakubaliana na wewe kwamba viongozi wanapaswa kuacha mtazamo walio nao na badala yake wakae na watu walaamu kama ninyi muwasaidie katika kushauri jinsi ya kuandaa mikakati ya kuongeza katika mustakabali wa ustawi .

 8. Paschal Florian

  Niuungane na wachezaji wote kwanza kupongeza mwandishi wa makala hii hoja yangu ni kwamba kwa mantiki hii bado inaonekana viongozi wana uchu wa madaraka ndiyo mana wanafanya vitu vya muda mfupi katika kipindi chao ili waendelee kuchaguliwa na pindi wanapomaliza siku zao za uongozi kila kitu kinaishia pale sasa je, sisi kama wanachi wazalendo tufanye nini katika kukutetea masilahi ya taifa letu.

 9. Asubuhi hii wakati napitia magazeti ya leo kwenye blog ya muungwana blog nimekutana na post hii ambayo kwakweli imenifanya nijione kama nimechelewa kukutana na hii Website yaani uchambuzi ulieoenda shule nilikuwa na kiu ya kukutana na watu kama hawa wenye uwezo wa kuona mbali kwa masilahi ya taifa.

 10. Swali langu mimi linalenga kwenye upande wa umeme wa jua kwa hiyo kuwekeza kwenye umeme wa jua kunaweza kuwa mkombozi wa badae katika ili swala la umeme na kama ndiyo ni namna gani tunaweza kufanya ili kuongeza nguvu katika eneo hili swali la pili ni aina gani umeme ambao serikali ikiwekeza inaweza kuokoa fedha na kuongeza upatikanaji wa umeme kwa muda mrefu.

  1. Peter Bujari MD

   Madam Anna: Mawazo yangu ni haya:
   1. Kuzalisha umeme cheap ambao long term production cost no ndogo. UK if any are hivi utauza umeme kwa bro no-go Sana. Maria Moreno hapa chini:
   a) Maeneo ya Ukanda wa Bahari na penye upepo mkali kama Makambako umeme wa uproot ndio cheapest. Norway, Denmark, Netherlands, Sweden wote hutumia umeme huo
   b) Mikoa yenye jua kali kama Singida, Ngoronngoro n. K umeme wa Joto
   c) Mikoa yenye makaa ya mawe umeme wa makaa ya mawe.

   Then kunakuwa na vituo vya kukusanyia na kuuza

 11. Athman Kapuya

  4th industrial revolution Ili ni neno jipya kwenye masikio yangu nimetamani kufuatili zaidi ili nielewe ukuaji wa viwanda na namna vinavyofanya kazi katika hatua za mabadiliko

  1. Peter Bujari MD

   Bwana Athmani. Karibu tujifunze wote. Jiandikishe tutakapoanza kufundisha masomo ya uongozi wenye tija

 12. Katika Nchi za Kiarabu kuna joto ambalo ni kali mara tatu au mbili ya joto la Dar Es Salaam lakini bado kuna nchi zinatumia umeme wa mafuta na sijasikia wakitangaza madhara kuzungumzia swala la umeme kwa taswira hii naona kama inaweza kuwa ni propaganda ni kwa mtazamo wangu

  1. Peter Bujari MD

   Bwana Abdul nimeaoma mtazamo wako. Uko sahihi na Huru kabisa. Jambo minimum siyo kujilinganisha na nchi za kiarabu ila ni kujua sayansi inaemaje? Mfano nchi za Kiarabu unazosema wanazalisha mafuta wenyewe, sisi tunanunua kwao. Je hesabu za kiuchumi hapo zinasemaje?

 13. Beatrice Eliya

  Kwa watu wachache ambao hawajaenda shule na wenye maono ya muda mfupi hawawezi kuelewa kilichoandikwa kwenye article hii lakini mimi nimeelewa na ninaunga mkono harakati hizi za kuangazia mazuri na changamoto zilizopo katika uongozi hii itasaidia hata viongozi kuelewa kwamba kuna watu wenye akili na mtazamo wenye manufaa kwa nchi yetu.

 14. Swaimece Mayeko

  Kupitia makala hii Nimeamasika kusoma masomo ya uongozi na nitajiunga na chuo mkianza masomo

 15. Amedeus Kimaro

  Nakumbuka Mchungaji Gwajima aliwahi kuongea maneno kama haya haya nimevutiwa zaidi kuyakuta katika namna ya uchambuzi wa kitaalamu na nimeelewa kwa upana nafikiri ni wakati wa viongozi kujitafakari na kutafuta namna ya kuanza upya kama hakuna pa kuendeleza.

  1. Peter Bujari MD

   @Amedeus nakushukuru. Mfano raisi amefukuza DC na DED wa Morogoro. Kisa waliwajengea wamachinga eneo la biashara lisilo na watu. Halafu wakigoma wanatuma mgambo kuwapiga. Viongozi wa aina hii ni wa hatari Sana. Kama huthamini watu unaowaongoza. Sasa unaongoza au unaua?

 16. Kwa maoni yangu naona serikali iwekeze katika vijana kuwaelimisha maana wao ndiyo watakao inuka na kuanza pale ambapo kwa nyakati zote hapakuwezekana katika viongozi waliopita vijana wana maana kubwa hata katika Biblia maana bado wana nguvu serikali ikiwatengenezea mazingira basi malengo yatatimia.

 17. Gustaph Lubida

  Unapozungumzia swala la magari yanayotumia uememe unatugusa wengi ambao tunatumia magari yanayo gharimu pesa nyingi kuweka mafuta kila siku na nilikuwa nawaza sana kwamba ili swala ipo siku litawezekana tutumie magari yenye umeme na sio mafuta

  1. Peter Bujari MD

   @Gustaph nashukuru kwa maoni yako. Swala la magari kutumia umeme linawezekana na limeisha anza kutumika. Magari huwa na battery ambazo huchajiwa kisha unaondoka. Hiyo ndiyo teknologia inayokuja. Unaweza kujifunza zaidi namna magari haya yanavyofanya kazi hapa
   https://www.power-and-beyond.com/

 18. Naunga mkono maoni ya kuwaendeleza vijana ao ndo watakuwa mkombozi wa kubadilisha mwelekeo ulipo sasa nafikiri viongozi wa sasa wanabidi kufumbua jicho la tatu kuwekeza katika vijana ili kuokoa maisha ya watu katika vizazi vinavyofuata.

  1. Peter Bujari MD

   @Sumo: Asante kwa hoja yako. Nakubaliana na wewe kuwa tuanze kuwekeza kwenye vijana. Hata hivyo tunahitaji mabadiliko kwenye mitaala ya shule za msingi kuanza kufundisha miiko ( Value) na kusaidia watoto kujua wao ni nani na thamani yao ni nini. Tukisubiri wakawa wakubwa, inakuwa vigumu kuwaondolea yale ambayo wanajua tayari.

 19. Godbless Katunzi

  Kwa mujibu wa mwandishi wa makala hii unaelezea vitu kwa utaalamu zaidi mimi natamani unifafanulie kitu kimoja kimoja kwa mfano 4th industrial revolution ikoje na revolution zilizotangulia pia zikoje?

 20. Julius Sigala

  Haya ndiyo mambo tunahitaji kwa nyakati hizi, kwa ajili ya masilahi ya taifa letu. Naunga mkono swala la kuendeleza vijana ili kuinua nguvu kazi ya badae na nafikiri tusisubiri serikali tuanze kuwawezesha vijana sisi wenyewe. Hayo ndiyo mawazo yangu.

 21. Nimejifunza mengi na kuimarika katika mafunzo haya ya high impact leadership incubator kikubwa nilichokiona hususani kwenye serikali yetu ya Tanzania tunaongozwa na siasa na sio malengo Wala miiko kila kiongoz anakuja na lake ingekuwa tuna viongoz watakao simamia malengo ya taifa na kila kiongoz mkuu anaye kuja anaendeleza pale mwezake alipoishia tungefika mbali na kuwa nchi yenye uchumi mzuri na WA kujitegemea mfano that late Magufuli aliwasimamisha kazi wenye vyeti feki Sasa hivi nasikia mchakato wa kuwarudisha hii inamaanisha hatuna lengo Moja la ataifa ila kila kiongoz anaamua lake kulingana na maslahi Yale binafsi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *