Bandari ya nne kwa ukubwa afrika kupewa kampuni tata ya dubai

Na. Mch. Dkt. Peter Bujari
bujari@peterbujari.com. June 13, 2023

Bandari aliyoanzisha Sultani Majidi Bin Said wa Zanzibar mwaka 1862 hatimaye yapewa Ahmed Mahboob Musabin”.

Kwa mujibu wa umoja wa bandari wa kimataifa, bandari ya Dar Es Salaam ni ya nne kwa ukubwa katika bara la Afrika, ikitanguliwa na Durban, Mombasa na Maputo. Kwa mujibu wa historia, bandari ya Dar Es Salaam ilianzishwa mwaka 1862 na Sultani wa Zanzibar Majid Bin Said, ila haikuendelea baada ya kifo chake. Bandari hiyo iliendelezwa na wajerumani miaka ya 1887 na baada ya uhuru ilikua ni mali ya serikali Tanganyika mpaka mwaka 2022. Baada ya mkataba tata kati ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, hali inategemewa kuwa tofauti.

Bandari hiyo imekuwa ikipanuliwa kwa vipindi tofauti kwa fedha za watanzania.  Kwa mujibu wa gazeti la Daily News March 19th, 2019 bandari ilikuwa iinapanuliwa kwa gharama ya dola za kimarekani million 421. Kwa mujibu wa mpango mkakati wa bandari ya Dar Es Salaam wa Julai 8th, 2020 jiwe la msingi liliwekwa ili kujenga bandari kavu kwa gharama ya dola za kimarekani million 20.  Uwekezaji wote huu inapewa kampuni iliyokataliwa marekani mwaka 2006 kupewa bandari kwa sababu za kiusalama. Raisi Bushi alipambana vilivyo kufanikisha hili, seneti ikasimama. Hata Tanzania tusimame kuzima mkataba huu.

Kwa mujibu wa mkataba tata (intergovernmental agreement) wa kiuchumi na kijamii uliosainiwa kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya dubai Octoba 25th, 2022, historia ya bandari ya Dar Es Salaam inabadilika milele. NDIYO MILELE. Mkataba huu una vifungu vingi ambayo vina utata, hauhitaji kuwa mwanasheria kuona hilo. Hata Bunge lililoridhia mkataba huu kwa madai kuwa ni kumuunga mkono Raisi, naona wamekwepa hoja. Majadiliano siyo kuhusu raisi, bali kuhusu vifungu vilivyomo katika mkataba. Raisi ni wa kwetu wote, ila akidanganywa na sisi lazima tumsaidie.Kumpenda kiongozi siyo kuunga mkono kila kitu, ni kumpa mawazo mapya na kumwonyesha kile asichokiona. Nithibitishe hoja yangu kwanini nasema bandari itamilikiwa milele.

Kifungu cha 23:4 kinasema kuwa pande zinazohusika hazitakuwa na haki ya kubatilisha, kujitoa, kusitisha au kuvunja mkataba katika mazingira yoyote hata wakikuka vifungu waziwazi, kubadilika kwa mazingira, kuvunjika kwa mahusiano ya ki-diplomasia, au sababu yoyote nyingine inayotambulika na sheria za kimataifa.

Kwa mijibu wa kifungu hicho mkataba huu ni wa milele kijamii na kiuchumi. Ndiyo maana nasema ni wa milele. Aliyeanzisha amechukua!. Wanaotetea mkataba huu wanasema walitembelea bandari ya dubai wakaona roboti zinaendesha bandari. Kwani Tanzania tumeshindwa nini kununua hiyo technlojia? Kwanini hawakuenda Mogadishu kujifunza, ? Hadidu rejea walizoenda nazo wabunge ziko wapi? Na taarifa yake iko wapi?. Kifungu 27 kinazuia Tanzania kuingia makubaliano ya ndani na ya nje na kampuni ama taasisi yoyote itakayokinzana na mkataba huu, kifungu hiki kinaoana ka kifungu 5:1 kinachoipa Serikali ya Dubai haki ya kipekee ( Exclusive rights). Je vyuo vikuu vya teknolojia ni vya kazi gani? Hivi kweli wabunge walisoma mkataba huu? Hivi kweli mwanasheria mkuu wa serikali alisoma mkataba huu? Hivi mkataba hii ulipita katika baraza la mawaziri?. Maswali ni mengi kuliko majibu. Na majibu mepesi kwa maswali magumu. Nipe mawazo yako kupitia bujari@peterbujari.com

50 thoughts on “Bandari ya nne kwa ukubwa afrika kupewa kampuni tata ya dubai”

 1. Mugisha bujari

  Ni kweli kabisa unachokisema nakuunga mkono by 100 percent.
  Inasikitisha jinsi ambavyo tunaona tunaenda kutawaliwa na bado tunakaa tunachekelea kama ni mazuri.
  Watu wanakaakugonga meza na kuingia kwenye magari makubwa without realising that in a few years to come all will be lost.
  We learnt neo-colonialism as a theory we never believed until it actually revealed itself in its truest form.

  Sasa sio wakati wa kuangalia vyama na mambo kama hayo. Tukiendelea hivi miaka 100 ijayo, we’ll have nothing to show our kids except history of a once peaceful nation.

  LET US STAND UP FOR OUR NATION!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *